Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015 taarifa zilienea kwamba msanii wa bongofleva Hussein Machozi amefariki kwenye ajali i...
Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015 taarifa zilienea kwamba msanii wa bongofleva Hussein Machozi amefariki kwenye ajali iliyohusisha gari la mizigo na gari dogo Dodoma.
Sauti ni ya Hussein mwenyewe, alipo pigiwa simu alianza kwa kusema ‘Nilijiandaa
hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye
charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana,
msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga
simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali
na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipo Dar es salaam‘
Kumbe baada ya taarifa za kifo kusambaa na
kuwafikia Mama yake mzazi pamoja na dada yake ambao walipiga simu yake
na haikupokelewa kwa muda mrefu, wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.
Sasa
hivi Hussein inabidi alazimike kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili
kuwahakikishia ndugu zake kwamba yuko hai manake aliongea kwenye simu ya
kaka yake na kumpa Dada simu baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.
COMMENTS