FORBES YATANGAZA ORODHA YA MATAJIRI WA AFRIKA MWAKA 2017

Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea iliyoandaliwa...



Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.
Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.

Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:

1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni

9. Isabel dos Santos, Angola

Utajiri: $3.1 bilioni

10. Issad Rebrab, Algeria

Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni

18. Folorunsho Alakija, Nigeria

Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni

20. Mohammed Dewji, Tanzania

Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni

Mada zinazohusiana

COMMENTS

Name

AJIRA AND SCHOLARSHIPS,3,CELLEBS,5,love tips,1,MAGAZETI,5,michezo,8,MIX-NEWS,11,New audio,36,politics,1,sports,4,stori za mapenzi,1,technology,1,video,28,
ltr
item
MSABAHA BLOG: FORBES YATANGAZA ORODHA YA MATAJIRI WA AFRIKA MWAKA 2017
FORBES YATANGAZA ORODHA YA MATAJIRI WA AFRIKA MWAKA 2017
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4sFhzoy9uKvv4uvycbwSSfVzXOM2hrx5nxYVKH6vVc-KAMmZVoHFX_FFhEmhR92IFgRmoLueQJz9Ysmev7MMfsKGHsVAbk7-i8_vBtqVjrx0uAffJab0lYbUNQWD5IGVbtanVlH7v2SgH/s640/DANGOTE.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4sFhzoy9uKvv4uvycbwSSfVzXOM2hrx5nxYVKH6vVc-KAMmZVoHFX_FFhEmhR92IFgRmoLueQJz9Ysmev7MMfsKGHsVAbk7-i8_vBtqVjrx0uAffJab0lYbUNQWD5IGVbtanVlH7v2SgH/s72-c/DANGOTE.jpg
MSABAHA BLOG
http://msabaha.blogspot.com/2017/03/forbes-yatangaza-orodha-ya-matajiri-wa.html
http://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/2017/03/forbes-yatangaza-orodha-ya-matajiri-wa.html
true
6741126810271918050
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy