Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbal, ambaye hivi karibuni alimgawia ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Pa...
Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbal, ambaye hivi karibuni alimgawia ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amehojiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Serikali.Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha jana kwamba mfanyabiashara huyo aliitwa kwa ajili ya mahojiano, lakini aliachiwa kwa dhamana baada ya muda kuonekana hautoshi.“Alikuja na wakili wake, lakini ameachiwa kwa dhamana ataripoti siku nyingine (hakutaja siku),” alisema Sirro.
“Anatuhumiwa kughushi nyaraka za
Serikali na sasa upelelezi unaendelea.”Mfanyabiashara huyo inadaiwa kuwa
aliripoti polisi jana saa tano asubuhi na kuhojiwa kabla ya kuachiwa
kwa dhamana jioni.Kuhojiwa kwa Ikbal, ambaye kampuni yake iliwahi
kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika miradi kadhaa
tata ya ujenzi, kumekuja siku chache baada ya kumgawia Makonda eneo la
ekari 1500 katika kitongoji cha Ligato kijiji cha Kisarawe II wilayani
Kigamboni kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo.
Siku mbili baadaye, Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliibuka na kueleza kwamba
eneo aliloligawa mfanyabiashara huyo si lake bali linamilikiwa na
serikali na wanakijiji.“Eneo lile ni la Serikali si la yule mtu
aliyejitangaza anampa Makonda na kwa sababu amemdanganya na mimi ndiye
msimamizi wa ardhi, nitamsaidia Makonda kuchukua hatua ili watu
wasijipendekeze kusafisha maovu yao kwa kutumia migongo ya viongozi,”
alisema Lukuvi.“Hadi siku ile alipokuwa anajipendekeza kwa Makonda,
ardhi ile haikuwa yake, wananchi walishashinda kesi mahakamani kwa
sababu hakuwa na vielelezo.
Ukimdanganya Mkuu wa Mkoa umeidanganya
Serikali. Makonda hakuomba ile ardhi ila yeye (Ikbal) ndiye alikwenda
kumgawia na amemgawia akijua kwamba alishashindwa kesi,” alisema
Lukuvi.Kwa mujibu wa hukumu ya kesi hiyo Na 147 ya mwaka 2015
iliyofunguliwa na Ikbal katika Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke dhidi
ya Baraza la Ardhi la Kijiji, mfanyabiashara huyo alishindwa.“Maombi
haya yanatupiliwa mbali pamoja na gharama,” ilisema hukumu hiyo ya
Januari 13, 2016.Ijumaa iliyopita mtu aliyejitambulisha kuwa ni
mwakilishi wa Ikbal, Kamugisha Katabaro aliibuka na kudai Lukuvi
amewasikitisha Watanzania na wataalamu mbalimbali wanaofahamu ukweli wa
jambo hilo.
Katabaro alidai Ikbal anamiliki ardhi
yenye ukubwa wa ekari 3,500 ambayo aliinunua tangu mwaka 2005 kutoka kwa
wananchi wa eneo la Lingato. “Wananchi waliliuza hilo eneo bila ya
kushurutishwa kwa kufuata taratibu za kisheria na umiliki wa ardhi,”
alidai.Mwananchi lilimfuata siku hiyo, Waziri Lukuvi aweke wazi kuhusu
mmiliki halali wa eneo hilo naye alisema,“Kama mfanyabiashara huyo
anaona ameonewa akate rufaa mahakamani.”Alisisitiza kuwa eneo hilo ni la
serikali na watu waliodhulumiwa wameanza kuorodhesha majina yao na
wataalamu wa ardhi wapo kwenye eneo hilo wakiendelea na upimaji.
“Hiyo ardhi ataipateje wakati mimi
ninayo, na kama ana nyaraka zinaonyesha ameshinda mbona hataki kuonyesha
anataka kuudanganya umma?” alihoji Lukuvi.Juhudi za kumpata Ikbal
hazikuzaa matunda lakini alipoulizwa Katabaro kuhusu mkurugenzi huyo
kuitwa polisi alisema ni kweli alitii wito kama alivyotakiwa na polisi.
Taarifa kwamba alikamatwa siyo za kweli kwani alihojiwa na kutoka jana
jioni baada ya kuwasili kituoni hapo saa tano asubuhi jana,”
alieleza.Eneo jingine ambalo Azimio ilizua utata ni umiliki wa ardhi na
uthaminishaji wake kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa uitwao
Dege Eco Village, Kigamboni. Ulisimama Februari mwaka jana kutokana na
utata wa ubia.
COMMENTS