MKASA WA KWELI! NI LAZIMA NILIPE KISASI TU! Naitwa Abdul Mazengo nimezaliwa katika mkoa wa Tabora miaka 28 iliyopita, ni mtoto w...
MKASA WA KWELI!
NI LAZIMA NILIPE KISASI TU!
Naitwa Abdul Mazengo nimezaliwa katika mkoa wa Tabora miaka 28
iliyopita, ni mtoto wa wa tatu katika familia yetu yenye watoto wanne.
Kama nilivyosema ni kwamba nimezaliwa huko tabora na kusoma huko huko
kuanzia darasa la awali mpaka darasa la kumi nambili baada ya hapo
nikachaguliwa kujiunga na shule ya kibaha, kwa ajili ya elimu ya juu,
ninamaanisha kidato cha tano na sita. Baada ya kihitimu kidato cha sita
nikarudi nyumbani kwetu Tabora kusubiri matokeo na baada ya kutoka
matokeo nilikuwa nimechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam
nikasoma kwa muda wa miaka mitatu na baada ya kumaliza masomo yangu
nikaajiliwa hapo hapo Dar. (samahani nimeficha majina yangu halali na
taarifa nyingine ni kwa sababu za usalama wangu!)
Nilifanya
kazi Dar kwa muda wa miaka miwili tu ndipo mnamo tarehe 5 January 2011
nikapata barua ya uhamisho wa kutoka Dar kuja huku Unguja ambako nipo
mpaka leo hii naendelea na kazi yangu. Ukweli ni kwamba nilishitushwa
sana na taarifa hiyo kwani ilikuwa ni ghafla mno. Na barua hiyo ilikuwa
inanitaka niripoti tarehe 08/01/2011 niwe tayari nimeshafika kwenye
kituo changu cha kazi, sio siri nilikuwa nimechanganyikiwa sana lakini
sikuwa na jinsi kama unavyoelewa serikali yetu ya Tanzania ilivyo,
utakachoagizwa lazima utekeleze kama alivyosema mkuu. Basi tarehe
6/01/2011 nikaanza safari yangu kutoka Dar kuelekea Zanzibar. Na kwa
sababu ilikuwa ni ghafla sana nilijitahidi kuchukua vitu vichache
ambavyo vilikuwa vya muhimu kwa wakati ule.
Basi niliondoka Dar
nikiwa na huzuni sana nikakata ticket then nikapanda boti na kuanza
safari yangu kuelekea Zanzibar. Kwa kweli nilifika salama nikatafuta
Guest moja, kesho yake asubuhi nikaanza kutafuta chumba cha kupanga,
sikupata shida kupata chumba ingawa nilikuwa sijawahi kufika Zanzibar
lakini pamoja na ugeni wangu nilibahatika kupata chumba haraka sana.
Baada ya kupata chumba nikaenda kuchukua mizigo yangu kwenye Guest House
niliyokuwa nimefikia na kuileta kwenye chumba changu, baada ya
kuhakikisha nimepanga kila kitu sawa sawia, nikaenda ufukweni kupunga
upepo na jioni nikarudi nyumbani kwangu.
Siku iliyofuata
ilikuwa ni tarehe 8/01/2011 ilikuwa ni siku ya kuripoti kazini kwangu
basi sikufanya ajizi nikiwa kama mfanyakazi mtiifu, nikaenda kuripoti
kazini na kwa bahati nzuri nilipokelewa vizuri na mkuu wangu wa kazi,
sio siri nilifurahi sana kwa namna ambayo nilipokelewa. Nikawa nimeanza
kazi sehemu yangu mpya ya kazi.
Pale nilipokuwa nimefikia
jirani kulikuwa na dada mmoja alikuwa anaitwa Noreen naweza sema kuwa
huyu alikuwa ndiye mwenyeji wangu kwa eneo hili maana yeye ndiye alikuwa
mtu wangu wa kwanza kabisa kuzoeana naye eneo lile. Noreen alikuwa
mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia ya mzee Hemmed Ramadan mwenyeji wa
kisiwa cha Pemba. Alikuwa anasoma chuo kikuu cha Zanzibar ( SUZA)
alikuwa anasomea Sheria mwaka wa tatu. Nooren alikuwa msichana mrembo
mrefu mwembamba, na mweupe kama ilivyo asili ya wasichana wengi wa
kipemba.
Ukweli ni kwamba nilizoeana na Noreen kwa muda mfupi
sana na tuliweza kuwa marafiki waliopendana kwa muda mfupi sana hii ni
kutokana na kwamba mtaani pale nilipokuwa nimepanga palikuwa hapana
mvulana ama kijana yeyote mwingine ambaye ningeweza kuongea naye kila
nilipokuwa nikitoka kazini. Hivyo nilimzoea sana Noreen naye pia
alinizoea kama kaka yake. Hivyo alikuwa akija ghetto kwangu kuongea na
wakati mwingine nilikuwa nikienda kwao.
Siku moja aliniomba
nimsindikize kwenye harusi ya rafiki yake ambapo yeye alikuwa anakwenda
kwa ajili ya kupiga picha za video. Sherehe iyo ilikuwa siku ya ijumaa
usiku na ilikuwa inafanyika SALAMA HALL Bwawani. Nilikubali kuwa pamoja
nae japo nilikuwa nimechoka lakini sikupenda kumuudhi rafiki yangu.Mnamo
majira ya saa 11jioni tuliondoka nyumbani kuelekea nyumbani kwa Bwana
harusi ambako ratiba nzima ilianzia hapo.
Noreen alivalia baibui la
blue maalum kwa hafla za usiku likiwa limenakishiwa kwa vito vya rangi
ya tanzanite.alivalia viatu virefu vya blue na mkoba wake wa begani pia
wa blue.alichukua mfuko mweusi kama begi ambako kulikuwa na moving
camera na taa yake kubwa. Mimi niliva suruali nyeupe ya kitamba,shati la
blue mikonc mirefu, tai ya rangi nyeupe yenye michirizi myeusi.chini
nilivaa 4 angle nyeusi. Tulitumia gari ambayo ilikodiwa maalum kwa ajili
ya mpiga picha.tukiwa njiani kuelekea kwa Bwana harusi maeneo ya kwa
MCHINA MWANZO tulikuwa tunataniana kama kawaida ya marafiki. Lakini
ghafla Noreen aliniuliza kama nimeoa. Nilipomwambia bado sijaoa
alifurahi sana na hata nilipomuuliza sababu ya kufurahi kwake
hakuniambia.
Tulipofika kwa Bwana harusi alipanga vifaa vyake
vizuri huku nikimsaidia kwa kufuata maelekezo yake. Hatimae majira ya
saa 1na 30 tuliondoka kuelekea ukumbini (Salama hall). Sisi
tulibadilishiwa gari na sasa tulitumia gari ya wazi ili tuweze kupata
picha nzuri ya maharusi. Gari yetu ilikuwa ikibadilika uelekeo kulingana
na maelekezo ya mpiga picha (Noreen)tulikuwa tukitangulia, mara
tunarudi nyuma ili kupata picha tofauti.
Saa mbili na robo
tulifika Bwawani,kwa hakika palipendeza sana.waalikwa wengi walikuwa
wameingia ukumbini na hata walioambatana na maharusi walitakiwa waingie
ndani,nje walibaki wasindikizaji wanne,watoto wawili wanaotangulia na
maharusi wenyewe.Sisi tulikuwa mbele kidogo ili tupate picha zao
wanapoingia na namna watu walivyojipanga ndani.Baada ya shughuli ya
maharusi kuingia kukamilika taratibu nyingine ziliendelea,lakini wakati
ratiba inafika mwisho na watu wanaondoka, Noreen alinitambulisha kwa
rafiki zake kuwa mimi ni mme wake mtarajiwa.sikuonesha dalili ya
kushtuka ingawa moyoni nilishtuka sana.tulisalimiana nao na kisha mimi
niliwaacha nikasogea pembeni.wakati tupo kwenye gari tunarudi nyumbani
(tulikuwa tunakaa daraja bovu karibu na gesti ya kwa mzushi) Noreen
aliniuliza nimejisikiaje kwa vile nilivyomsaidia ktk upigaji picha.
Nilimjibu kuwa nimefurahi kwa kupata mwalimu wa kunifundisha taalum
nyingine.kisha akaniuliza tena kama nilichukia aliponitambulisha kuwa
mimi ni mme wake mtarajiwa nilimwambia sijachukia wala sintoweza
kuchukia zaidi ya kuomba iwe kweli.alicheka sana. Tulipofika nilimpeleka
kwao kwanza then mimi nikaenda zangu kulala.lakini nilipoingia ndani
Noreen alinipigia simu na kuniuliza kama nimechoka sana nikamjibu
sijachoka,akaniambia kuna kitu anataka kuniambia kama naweza kumsikiliza
kwa muda huo. Nilimjibu muda upo wa kutosha labda yeye awe amechoka tu.
COMMENTS