''Ozil ajutia kukosa penalti'' Wenger 21 Februari, 2014 - Saa 11:43 GMT ...
21 Februari, 2014 - Saa 11:43 GMT
Ozil ajuta kukosa penalti
Kocha wa Arsenal ya Uingereza
Arsene Wenger, amesema kuwa mshambulizi Mesut Ozil angali anajutia
kukosa kufunga penalti dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu barani
ulaya Bayern Munich jumanne iiyopita.
Ozil, mwenye umri wa miaka 25,alilazimika kuwaomba radhi mashabiki wa Arsenal kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.Ozil,alisajiliwa mapema msimu huu kwa kitita kikubwa zaidi na kocha Wenger.
Arsenal, inashikilia nafasi ya pili katika ligi kuu ya premia ya Uingereza ikiwa na jumla ya alama 56 moja nyuma ya vinara Chelsea .
Arsenal inaikaribisha Sunderland jumamosi katika uwanja wa Emirati
COMMENTS