Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu

Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu  2 Machi, 2014 - Saa 13:09 GMT ...

Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu

 2 Machi, 2014 - Saa 13:09 GMT
Andre Schurrle mchezaji wa Chelsea
Timu ya Chelsea imezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya kuicharaza Fulham magoli 3-1 na kujikusanyia pointi 63.
Mabao yote matatu ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji wake Andre Schurrle akiyafunga katika dakika ya 52, 65 na 68, huku bao la kufutia machozi la Fulham likifungwa na Heitinga katika dakika ya 74.
Arsenal iliyokuwa ikifukuzana na Chelsea kwa tofauti ya pointi moja imejikuta ikiachwa pointi nne zaidi baada ya kucharazwa na Stoke goli 1-0. Arsenal imebaki na pointi 59 na kuporomoka hadi nafasi ya tatu, huku Liverpool ikipanda, nayo ikiwa na pointi 59 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga.
Wakati Newcastle ikiididimiza Hull kwa mabao 4-1, nayo Everton iliibanjua West Ham bao1-0.
Msimamo wa ligi kuu ya England baada ya michezo hiyo ya Jumamosi, Chelsea inaongoza kwa pointi 63 baada ya kucheza michezo 28 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 59 na Arsenal ni ya tatu ikiwa pia na pointi 59.
Mancity ni ya nne ikiwa na pointi 57 lakini ikiwa imecheza michezo 26 tu, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kwenda kileleni iwapo itashinda mechi zake mbili.
Manchester United mabingwa watetezi, iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 45 lakini imecheza michezo 27.
Mkiani kabisa ni Fulham yenye pointi 21 na mbele yake ni Cardiff yenye pointi 22.

COMMENTS

Name

AJIRA AND SCHOLARSHIPS,3,CELLEBS,5,love tips,1,MAGAZETI,5,michezo,8,MIX-NEWS,11,New audio,36,politics,1,sports,4,stori za mapenzi,1,technology,1,video,28,
ltr
item
MSABAHA BLOG: Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu
Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/03/01/140301164231_andre_schurrle_chelsea_304x171_afp_nocredit.jpg
MSABAHA BLOG
https://msabaha.blogspot.com/2014/03/chelsea-yajiimarisha-kileleni-ligi-kuu.html
https://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/2014/03/chelsea-yajiimarisha-kileleni-ligi-kuu.html
true
6741126810271918050
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy