Oscar hatiani kwa kuua bila kukusudia oscar akibubujikwa na machozi mahakamani ...
Oscar hatiani kwa kuua bila kukusudia
oscar akibubujikwa na machozi mahakamani
Oscar Pistorius leaves the High Court in Pretoria after the verdict in his murder trial Photo: Gianluigi Guercia/AFP/Getty Images
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp pasi na kukusudia.
Akitoa
uamuzi wake jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua
Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa
choo akiwa akatika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa
amevamia nyumba yake.Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp na kwamba alifanya mauaji hayo kwa kusudi.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani.
Jaji Thokozile Masipa amesogeza muda wa mwanaridha huyo yuko huru kwa dhamana.
Pistorius atakuwa huru hadi hukumu itakapotolewa mwezi ujao, ambapo anaweza kuhukumiwa hadi miaka 15 gerezani. Oscar Pistorius ataendelea kukaa kwa mjombake alikokuwa muda wote kesi ilipokuwa ikiendelea.
Mjombake Pistorius, Arnold Pistorius amemshukuru Jaji Masipa kwa uamuzi wake wa kumuachia kwa dhamana.
tizama video hii wakati kesi ikisomwa
COMMENTS