Z Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeshika nafasi ya kumi miongoni mwa vyuo vikuu 50 bora na vyenye umaarufu Afri...
Z
Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeshika nafasi ya kumi miongoni mwa vyuo vikuu 50 bora na vyenye umaarufu Afrika.
Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeshika nafasi ya kumi miongoni mwa vyuo vikuu 50 bora na vyenye umaarufu Afrika.
Kadhalika UDSM kimetajwa kuwa miongoni mwa chuo vikuu chenye idadi kubwa ya wanafunzi na walimu na wingi wa programu za masomo.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza
Mukandala alisema chuo hicho kina haki ya kushika nafasi hiyo kutokana
na jitihada zinazofanywa na uongozi.
“Tulifanya jitihada kuhakikisha tuna walimu wazuri
wenye shahada za uzamili na uzamivu, maabara nzuri na miundombinu
rafiki ya kufundishia,” alisema Mukandala.
Alisema UDSM ina mitaala bora inayoendana na wakati na inazalisha wataalamu wengi kwa mwaka.
“UDSM inachaguliwa na wanafunzi wengi na pia ina wanafunzi wa kimataifa,”alisema.
Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa na
Taasisi ya Kimataifa ya Vyuo Vikuu na vya Kati (4ICU) ya Uingereza, chuo
hicho kilishika nafasi ya 10 kati ya vyuo 50 vilivyopimwa kulingana na
vigezo vya taasisi hiyo.
Hata hivyo, taasisi hiyo ilieleza kuwa hawapimi
ubora wa vyuo kwa kuangalia kiwango cha elimu inayotolewa au huduma bali
wanaangalia umaarufu wa chuo kimataifa.
“Huu mtandao si kwa ajili ya taaluma wala
usichukuliwe kama kipimo cha kuchagua programu au nafasi ya masomo, huu
ni kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kimataifa kufahamu jinsi taasisi
ya elimu ilivyo maarufu katika nchi nyingine,” ilisema taarifa ya 4ICU.
Katika taarifa hiyo, Chuo Kikuu cha Cape Town cha
Afrika Kusini kilishika nafasi ya kwanza huku vingine vilivyoshika tano
bora vikitoka nchini humo.
Nafasi ya pili ilishikwa na Chuo Kikuu cha
Pretoria, ya tatu Chuo Kikuu cha Stellenbosch na nne ilikwenda kwa Chuo
Kikuu cha Witwatersand na tano ikishikwa na Chuo Kikuu cha Afrika
Kusini.
Ikieleza namna walivyoweza kupata vyuo bora,
tovuti ya 4ICU iliangalia jinsi mitandao mingine inavyozungumza na kutoa
taarifa za chuo husika, nafasi yake katika kurasa za mtandao ya kijamii
kutafuta taarifa kwa google, chuo kinavyotumiwa kama rejea katika
taarifa mbalimbali na ni kwa kiasi gani watu wanaitumia tovuti ya chuo
husika. chanzo
COMMENTS