Baada ya msanii wa filamu za vichekesho Steve Nyerere kuambiwa yeye ni panya na TID, muigizaji huyo ameibuka na kujibu mapigo.Wawili hao...

Muigizaji huyo alidai yeye hawezi kuanza kujibishana na TID kwa kuwa TID si kitu chochote.
“Siwezi kubishana na TID ambaye akiona
gari yangu analikimbia apate chochote kitu. Kwahiyo nikianza kubishana
naye nitakuwa napoteza muda, halafu mimi na TID ni kama vidole kuna
kikubwa na kidogo yeye wakati wake ulishapita huu ni wakati wa Steve
lazima ajenge heshima,” Steve Nyerere alikiambia kipindi cha Enewz cha
EATV.
Aliongeza “Alivyonifananisha na panya
nimependa kweli, kwanza namsifu kwa sababu amenifananisha na kiumbe
mjanja. Kwahiyo mimi nasema bora mimi panya kuliko yeye paka ambaye
anasubiri atengewe ale, nimefurahi sana kwa sababu amenisifia
kunifanisha na mnyama mjaja,”.
Kuhusu issue na kuburuzwa mahakamani kwa
tuhumu alizozitoa dhidi ya TID, Steve Nyerere ameomba radhi kwa kauli
ile huku akidai tayari alishaomba msahama mbele ya waandishi wa habari
kwa wote aliowazungumzia kwenye audio ambayo ilisambaa mitandaoni.
COMMENTS