Marekani:kemikali ilitumika kuuwa Syria

Marekani:kemikali ilitumika kuuwa Syria

Marekani:kemikali ilitumika kuuwa Syria  26 Agosti, 2013 -...


Marekani:kemikali ilitumika kuuwa Syria

 26 Agosti, 2013 - Saa 19:57 GMT
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry
Waziri wa Mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani, John Kerry ameshtumu anachokitaja kama hatua ya serikali kutumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake kama ukosefu wamaadili wa hali ya juu.
Amesema kanda za video za silaha zinazotuhumiwa kuwa za kemikali karibu na mji wa Damascus ni kweli na zisizoweza kukanushwa.
Kerry aliongezea kwamba Rais Barack Obama anatafakari hatua ya kuchukua.
Haya yanajiri saa chache baada ya wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa kushambuliwa karibu na mji mkuu huo.
Wachunguzi wa silaha za Umoja wa mataifa kuwasili katika eneo lililopo viungani mwa mji mkuu Damascus ambapo inashukiwa kuwa wiki iliyopita kulishambuliwa kwa silaha za kemikali .
Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wanasema wachunguzi hao wa Umoja wa mataifa wanakutana na waathiriwa wa shambulio linaloshukiwa kuwa ni la gesi ya sumu na madaktari waliowatibu .
Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wa silaha za kemikali
Wachunguzi hao watachunguza mabaki na kukusanya sampuli za udongo, damu na tishu kwa ajili ya vipimo vya maabara. .
Awali watu wasiojulikana wenye silaha waliushambulia kwa risasi msafara wa magari waliokuwemo wakaguzi hao walipokuwa wakielekea kwenye eneo la tukio - na kuwalazimisha kurejea nyuma kwa muda .
Vyombo vya habari vya kitaifa nchini viliwashutumu waasi kufanya shambulio hilo.
Rais Assad aliwaruhusu wakaguzi wa silaha baada ya kukabiliwa na shinikizo kubwa la kimataifa, lakini Marekani na Uingereza zimesema ushahidi mwingi huenda uliharibiwa katika muda wa siku tano, tangu kutokea kwa mashambulio.
Wakati huo huo serikali za magharibi zimeikosoa Syria kwa kuchukua muda mrefu kuruhusu timu ya Umoja wa mataifa ya wakaguzi wa silaha kuzuru eneo linalodaiwa kushambuliwa kwa silaha za kemikali na zinaangalia uwezekano kuingilia kati kijeshi nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

Name

AJIRA AND SCHOLARSHIPS,3,CELLEBS,5,love tips,1,MAGAZETI,5,michezo,8,MIX-NEWS,11,New audio,36,politics,1,sports,4,stori za mapenzi,1,technology,1,video,28,
ltr
item
MSABAHA BLOG: Marekani:kemikali ilitumika kuuwa Syria
Marekani:kemikali ilitumika kuuwa Syria
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/26/130826194116_syria_kerry_512x288_bbc_nocredit.jpg
MSABAHA BLOG
https://msabaha.blogspot.com/2013/08/marekanikemikali-ilitumika-kuuwa-syria.html
https://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/2013/08/marekanikemikali-ilitumika-kuuwa-syria.html
true
6741126810271918050
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy