ARSENAL HAIKAMATIKI LIGI KUU ENGLAND CHINI YA WENGER

ARSENAL HAIKAMATIKI LIGI KUU ENGLAND CHINI YA WENGER

 2 Januari, 2014 - Saa 12:06 GMT Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walc...


 2 Januari, 2014 - Saa 12:06 GMT
Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott

Ligi kuu ya England inazidi kupamba moto, huku Arsenal wakiendelea kukalia kiti cha uongozi, baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Cardiff City. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, anasema:
"Tunajua tutacheza michezo 10 hapa nyumbani na tunataka kuifanya sehemu hii kuwa ngome yetu, bila kujali wengine wanafanya nini.
"Iwapo tunaweza kufanya hivyo, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi."
Arsenal, haiko salama sana katika nafasi yake ya kwanza ikiwa na pointi 45, kwani kwa karibu sana inanyemelewa na Manchester City yenye pointi 44, huku Chelsea ikiweka kibindoni pointi 43 ikiwa katika nafasi ya tatu. Liverpool imejisogeza juu kutoka nafasi ya tano sasa iko nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi 39, huku Everton ikipigwa kumbo na kusogezwa nafasi ya tano kwa kuwa na pointi 38. Wakati Tottenham ikipanda juu katika nafasi ya sita kwa kupata pointi 37, mabingwa watetezi Manchester United imesukumwa chini hadi nafasi ya saba kwa kukusanya pointi 34.
Wakati timu hizo zikipigana kufa kupona kunyakua ubingwa wa ligi kuu au kuwemo katika nne bora, timu nyingine zinapigana kuepuka kushuka daraja. Timu zilizo katika hatari zaidi mpaka sasa baada ya timu zote kucheza mechi 20, ni Sunderland iliyoko nafasi ya 20 kati ya timu 20 za ligi hiyo,ikiwa na pointi 14 tu. West Ham inashikilia nafasi ya 19 ikiwa na pointi 15 na Crystal Palace ni ya 18 ikipata pointi 17 na kuipisha Cardiff City katika nafasi ya 17 iliyokuwa inashikilia kabla ya mchezo wa Jumatano.

Taarifa zinazohusiana

Name

AJIRA AND SCHOLARSHIPS,3,CELLEBS,5,love tips,1,MAGAZETI,5,michezo,8,MIX-NEWS,11,New audio,36,politics,1,sports,4,stori za mapenzi,1,technology,1,video,28,
ltr
item
MSABAHA BLOG: ARSENAL HAIKAMATIKI LIGI KUU ENGLAND CHINI YA WENGER
ARSENAL HAIKAMATIKI LIGI KUU ENGLAND CHINI YA WENGER
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/01/01/140101163321_arsenal_walcott_304x171_reuters_nocredit.jpg
MSABAHA BLOG
https://msabaha.blogspot.com/2014/01/arsenal-haikamatiki-ligi-kuu-england.html
https://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/2014/01/arsenal-haikamatiki-ligi-kuu-england.html
true
6741126810271918050
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy