Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani wamechuana mahakamani katika kesi ya ...
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani wamechuana
mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge huyo na wahariri
wa gazeti la Mawio.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu Thomas
Simba leo atatoa uamuzi wa kama Hamdani aeleze anachokifahamu juu ya
Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC), Jecha Salim Jecha anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.
Hiyo ilikuwa ni baada ya Lissu kumtaka
Hamdani,ambaye ni shahidi wa upande wa mashtaka, aeleze anachokifahamu
kuhusu Katiba ya Zanzibar na kama Jecha anaweza kufuta matokeo ya
uchaguzi.
Hakimu Simba alifikia uamuzi huo baada
ya wakili wa Serikali, Paul Kadushi kupinga shahidi huyo kujibu swali
hilo kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala katiba hivyo hawezi kutoa
tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba.
Lissu alimhoji Hamdani maelezo yake yaliyo polisi aliyaandika kama nani? Mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Hamdani: Niliandika maelezo yangu kama mlalamikaji na kwamba mikusanyiko hiyo haikuwa haramu, ilikuwa halali kisheria.
Lissu: Mweleze mheshimiwa kama mihemko kisheria inakatazwa ama la?
Hamdani: Haikatazwi
COMMENTS