Mh Zitto Kabwe ....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua Kuhusu ufisadi wa IPTL
HomeMIX-NEWS

Mh Zitto Kabwe ....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua Kuhusu ufisadi wa IPTL

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameendelea kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya anachokiita uf...

Hivi ndivyo mh. Ridhiwani Kikwete alivyosema dhidi ya shutuma ya kuhusika na Madawa
MAZITO YAMEJILI KWENYE KESI YA TUNDU LISSU MAHAKAMANI HIVI LEO
MAGUFULI AMEPATA USHINDI WA ASILIMIA 100 KUWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA
Tokeo la picha la zito kabwe bungeni leo

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameendelea kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya anachokiita ufisadi katika kampuni ya uzalishaji umeme ya IPTL, inayomilikiwa na Kampuni wa PAP.

Tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka 2015, Zitto amekuwa mstari wa mbele kumsihi na kumuomba Rais Magufuli afanye maamuzi juu ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikilipwa milioni 300 kila siku bila kujali kama inazalisha umeme au la.

Kupitia mitandao ya kijamii, Zitto ameandika "Rais John Magufuli ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka mwaka 1995. watanzania masikini na wanyonge tutakuwa nyuma yake kwenye hili. Atende sasa."

Mnamo tarehe 21, Septemba 2016 Mhe. Zitto Kabwe alimtaka tena Rais Magufuli aoneshe hasira zake dhidi ya hicho anachokiita ufisadi mkongwe wa IPTL huku akieleza masikitiko yake juu ya kutochukuliwa kwa hatua zozote hadi sasa.

Mhe. Zitto Kabwe ambaye amekuwa hachoki kulizungumzia sakata hilo la IPTL amehoji ni nini kipo nyuma ya pazia, na ni nani mfaidika hadi hatua zisichukuliwe, huku akitoa ushauri wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mahakama kwa sasa.

"Mahakama Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa. Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m kila siku izalishe au isizalishe umeme? Ushahidi wote ulionyesha utapeli wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha uamuzi wa Mahakama umefanya matapeli hawa kuendelea kunyonya fedha kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc? Ama ni jipu la mgongoni?". Alihoji Mhe. Zitto Kabwe
Name

AJIRA AND SCHOLARSHIPS,3,CELLEBS,5,love tips,1,MAGAZETI,5,michezo,8,MIX-NEWS,11,New audio,36,politics,1,sports,4,stori za mapenzi,1,technology,1,video,28,
ltr
item
MSABAHA BLOG: Mh Zitto Kabwe ....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua Kuhusu ufisadi wa IPTL
Mh Zitto Kabwe ....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua Kuhusu ufisadi wa IPTL
https://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/03/KABWE.jpg
MSABAHA BLOG
https://msabaha.blogspot.com/2017/02/mh-zitto-kabwe-amtaka-rais-magufuli.html
https://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/
http://msabaha.blogspot.com/2017/02/mh-zitto-kabwe-amtaka-rais-magufuli.html
true
6741126810271918050
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy